Jumuiya ya Watu wenye Uwalbino Zanzibar (JWUZ) wameshauriwa kuzijali sana Afya zao na kuzitunza vyema Ngozi zao hususani katika kipindi cha Jua kali ili kujiepusha na Maradhi ya Ngozi na Magonjwa mengine.
Hayo ameyasema Daktari Bingwa wa maradhi ya ngozi Dr Hafidh S. Hassan katika Clinic ya maradhi ya Ngozi Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati akitoa huduma kwa wagonjwa wa matatizo ya ngozi wakiwemo Albino.
Aidha Dr. Hafidh amegawa baadhi ya Vifaaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili ya kujikinga na mwanga mkali wa Jua ikiwemo miwani,kofia pamoja na lotion ambavyo ni muhim kwao kwani Jua huathiri Ngozi zao na Macho.
Nao Viongozi wa Jumuiya hiyo wamewaomba washiriki wenzao kujitokeza kwa wingi katika Clilic yao kwani wanapata kujifunza mambo mengi yanayohusiana na matatizo ya ngozi hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Daktari Bingwa wa Maradhi ya Ngozi Dr Hafidh S. Hassan, akitoa maelekezo namna ya kujikinga juu ya maradhi ya Ngozi.
Baadhi ya watu waliofika katika Clinic ya Ngozi hospitali ya Mnazi Mmoja wakitoa shukurani za dhati kwa Uongozi wa Hospitali na Madakitari kwa huduma wanazozipata wanapofika clinic.