Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja watakiwa kubadilika na kufanya Kazi kwa bidii ili kuimarisha huduma kwa wanao wahudumia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dr.Msafiri L. Marijani wakati akifungua Mafunzo ya Wafanyakazi yanayotolewa na Kitengo cha huduma kwa Mteja yaliyofanyika katika Ukumbi wa Bohari ya madawa ya Hospital hiyo.
Dr Marijani amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uwezo wa utendaji kazi kwa Wafanyakazi hivyo wanatakiwa kuyatumia Mafunzo hayo kwa kutoa mabadiliko chanya ambayo yataimarisha Huduma na kupunguza baadhi ya changamoto zinazojitokeza mara kwa mara kati ya Watoaji Huduma na wanaoihitaji huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambae ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja na Msemaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Hassan Makame Mcha amesema kuwa amewapa Mafunzo hayo Wafanyakazi ili kuimarisha Mawasiliano mazuri na Wanajamii pale wanapohitaji Huduma.
Kwa upande wa Washiriki wa Mfunzo hayo wamesema wameyapokea Mafunzo hayo na kuahidi kubadilika na kuleta Maendeleo ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Mafunzo hayo yametolewa na Kitengo cha Huduma kwa Mteja yalioyowashirikisha Viongozi wakiwemo Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wauguzi wa hospitali ya mnazi.
Dr. Msafiri L. Marijani akisisitiza umuhim wa kuyafahamu mafunzo hayo na kuyafanyiakazi kwa wafanyakazi wa Hospitali kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma mzuri wagojwa wanaofika Hospitali.