Madaktari na Wauguzi wa Wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mnazi mmoja wamepatiwa mafunzo ya kutumia kifaa kipya cha kitaalamu cha kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto tumboni kwa mama kinachoitwa MOYO FETAL HEART RATE MONITOR kifaa ambacho kitasaidia kujua mapigo ya moyo na hali ya mama wakati wanapokua na uchungu.
Muuguzi dhamana wa wodi ya wazazi Magret S. Taayari amesema kuwepo kwa kifaa hicho kitasaidi kuokoa muda kutokana na urahisi wa matumizi yake kulinganisha na kifaa cha zamani ambacho hutumia muda mwingi kuangalia mapigo ya moyo ya mtoto na mama.
Mafunzo hayo yametolewa na muuguzi wa Watoto Gunnelin Ueivog kutoka chuo Kikuu cha Haukland cha Nchini Norway ambapo yalifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dr. Msafiri Marijani.