Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Muwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania, Bi Theresia Mcha,alipowasili katika viwanja majengo hayo kwa ajili ya uzinduzi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Ki+kuu cha Haukeland Norway Bwa. Eivind Hansen. wakikata utepe kuashiria kulizindua jengo la Wodi ya Watoto katika eneo la hospitali ya Mnazi Mmoja litakalotoa huduma kwa Watoto na Wazazi katika hospitali hiyo Zanzibar.
Jengo Jipya la Wodi ya Watoto katika hospitali ya Mnazi Mmoja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimsikiliza Muunguzi wa Wodi ya Wazazi akitoa maelezo ya moja ya mashine za kisasa katika jengo hilo zitakazotumika kutowa huduma kwa Wamama Wajawazito katika Wodi hiyo.