matangazo

matangazo (9)

saratani 4

SERIKALI YA MAPIDUZI ZANZIBAR YA AWAMU YA NANE INADHAMIRA YA DHATI KABISA YA KUJENGA KITUO KIPYA CHA MARADHI YA SARATANI KWA VIFAA BORA VYA UHAKIKANA VYA KISASA.

AMEYASEMA HAYO WAZIRI WA AFYA USTAWI WA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE.NASSOR MAZRUI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI DUNIANI (WORLD CANCER DAY) YALIYOFANYIKA KATIKA KITENGO CHA MARADHI YA SARATANI NDANI YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA.

AMESEMA LENGO LA MAADHIMISHO HAYO NI KUKAA KWA PAMOJA NA WATAALAMU WA MARADHI HAYO NA KUJUA NAMNA YA KUJIKINGA NA MARADHI YA SARATANI KWANI KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

HATA HIVYO AMEWAOMBA WANANCHI WANAPOHISI HALI YA UTOFAUTI KATIKA MWILI AU UVIMBE WOWOTE WAFIKE KITUO CHA AFYA KWAAJILI YA UCHUNGUZI.

NAE MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA AMBAE PIA NI DAKTARI BINGWA WA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA SARATANI MSAFIRI L. MARIJANI, AMEELEZA UGONJWA WA SARATANI NI UGONJWA UNAOCHUKUA NAMBA MBILI DUNIANI UNAOPELEKEA KIFO KWA MUATHIRIKA HIVYO HOSPITALI INAJITAHIDI KWA KIASI KIKUBWA KUTIBU UGONJWA HUO KWA MUDA MUAFAKA INGAWA GHARAMA ZA VIPIMO NA MATIBABU KWA WAGONJWA WA SARATANI NI KUBWA SANA.

AMEISHAURI JAMII IWE NA UTARATIBU WA KUCHANJA CHANJO HUSUSANI CHANJO DHIDI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 13 ILI KUUWA BAKTERIA WANAOATHIRI SHINGO YA KIZAZI.

MUAKILISHI WA BALOZI WA NCHINI UTURUKI KUTOKA TANZANIA BARIS OZYURT AMBAE NI MKURUGENZI WA TUKRISH MAARIF SCHOOL,AMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUPATIWA HUDUMA YA KIMATIBABU PIA AMETAJA VIDOKEZO VINAVYOPEKEA KUPATA UGONJWA WA SARATANI ,UNENE ULIOKITHIRI,UKOSEFU WA MAZOEZI,UTUMIAJI WA TUMBAKU,POMBE NA JAMBO KUBWA LA MSONGO WA MAWAZO(STRESS)

MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI HUAZIMISHWA KILA KILA IFIKAPO FEBRUARI 04 YA KILA MWAKA AMBAPO KAULI MBIU YA MWAKA HUU…IMARISHA HUDUMA ZA SARATANI ZIWAFIKIE WOTE.

saratani 12

DSC 0503

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr.Hussein Mwinyi ameipongeza taasisi ya  LADY FATMA FOUNDATION kwa msaada wake wa huduma ya maji katika Hospitali ya Mnazi mmoja .

Dr. mwinyi alisema kuwa ni Habari njema kuona kuwa kupitia mradi huo sasa hospitali inauwezo wa kuzalisha lita 240,000 kwa siku moja ikiwa mahitaji ni lita 400,000 ambapo tayari umeshaipunguzia mzigo mkubwa mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA hasa pale miundombinu ya maji inapoharibika.

Rais Dr. Mwinyi alitoa pongezi kwa taasisi hiyo kwa kuratibu na kutafuta wafadhili wa mradi huo na kuchimba visima, pia aliipongeza kampuni ya DEG ya Ujerumani kwa kuleta Mitambo ya kuchuja chumvi na Mitambo ya kuzalisha umeme wa jua ambao utatumika katika Mtambo huo wa kusafisha maji chumvi na kuwa maji salama.

Waziri wa Afya, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema mtambo huo umekuja muda muafaka kutokana na kuwepo upungufu wa maji kutoka ZAWA na kupelekea hospitali kuwa na upungufu wa maji hivyo kuchimbwa kwa Visima hivyo Pamoja na kuwepo kwa mtambo wa kuchujia maji ya chumvi na kuwa maji salama utasaidia sana upatikaji wa maji ndani ya  Hospitali.

m 20

m 15

DSC 0459

m 19

 m 18

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi amempongeza mwekezaji mzalendo Mohamed Abdallah Mohamed ambae pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Zanzibar Cable Television kwa kujitolea kujenga jengo la kuhifadhia maiti MOYUARY katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

Dr. Mwinyi amesema juhudi za muekezaji huyo zimechochea ari na hamasa ya wafanyabiashara wenzake na wananchi wengine kujitolea kutoa misaada ya kijamii.

Amesema ujenzi huo wa chumba cha kuhifadhia maiti chenye majokofu Matano na uwezo wa kuhifadhi maiti 20 kwa wakati mmoja unathaminiwa sana ambapo kutaweza kuhifadhiwa maiti kunapotokezea majanga mbali mbali ikiwemo vifo vyenye utata na ajali.

Daktari bingwa wa vifo vinavyotokana na Jinai Dr. Wardat Attai Masoud amesema Hospitali imekuwa na jukumu kubwa la kufanya upasuji wa vifo vyenye utata, ajali na vile vinavyotokana na jinai kwa kiasi kukibwa kutokana na engezeko la kesi hizo na kwa wale ambao bado hawajajulikana jamaa zao huhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mnazi mmoja ambacho kilikua na changamoto kadhaa hivyo kuwepo kwa jingo hilo lenye maeneo ya nafasi litasaidia kwa kiasi kikubwa kwa hospitali.

m 26

Mh.Waziri wa Afya Usitawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Bwana Nassor Ahmed Mazorui amesema sasa hospitali imeshakuwa na nafasi yakutosha ya kuhifadhi Maiti, maiti zinaweza kuhifadhiwa vizuri.

m 1

m 12

m 29

MOYO K 5

Madaktari na Wauguzi wa Wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mnazi mmoja wamepatiwa mafunzo ya kutumia kifaa kipya cha kitaalamu cha kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto tumboni kwa mama kinachoitwa MOYO FETAL HEART RATE MONITOR kifaa ambacho kitasaidia kujua mapigo ya moyo na hali ya mama wakati wanapokua na uchungu.

Muuguzi dhamana wa wodi ya wazazi Magret S. Taayari amesema kuwepo kwa kifaa hicho kitasaidi kuokoa muda kutokana na urahisi wa matumizi yake kulinganisha na kifaa cha zamani ambacho hutumia muda mwingi kuangalia mapigo ya moyo ya mtoto na mama.

Mafunzo hayo yametolewa na muuguzi wa Watoto Gunnelin Ueivog kutoka chuo Kikuu cha Haukland cha Nchini Norway ambapo yalifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dr. Msafiri Marijani.

MOYO K 19

 

 

MTOTO MACHO 2

Kuwepo kwa vifaa vya kutosha na Madaktari Bingwa katika kitengo katika cha Macho kutaboresha huduma za kimatibabu kwa urahisi kwa Wagonjwa wetu.

Hayo yameelezwa na Daktari Mkuu wa Kitengo cha Macho ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dk Slim Mohammed Mgeni katika siku ya kufunga kambi ya matibabu ya macho kwa Watoto.

Kambi hiyo imefadhiliwa kwa udhamini wa lions club -mzizima Dar-es salam kwa lengo la kutoa huduma za kimatibabu na kuisaidia jamii kupata matibabu ya macho kwa Watoto bila malipo.

Aidha Dk, Slim amesema wagonjwa waliopatiwa matibabu walikua 360 kwa maradhi tofauti yakiwemo presha ya macho,kensa ya macho,makengeza,macho yanayohitaji miwani na maradhi mengine ya macho ikiwemo kufanyiwa upasuaji kwa waliohitaji huduma hiyo.

Nae Muakilishi wa Jumuiya iyo ya Lions club Mohamed Rasulullah kwa niaba ya Jumuiya hiyo amesema wameona ni vyema kutoa huduma ya macho bila malipo kwani Watoto wengi hupata matatizo na baadae wazazi kushindwa kuwahudumia Watoto wao ndio maaana wameamua kutoa huduma hiyo kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Muhimbili Pamoja na madaktari bingwa wa hospitali ya mnazi mmoja.

macho 2 6 2

Muakilishi wa Jumuiya ya Lions club Mohamed Rasulullah akitoa neno la shukurani kwa Uongozi wa HOSPITALI kwa namna walivyopata mashirikiano katika kipindi chote cha KAMBI ya matibabu hayo.

macho 7 6 2 2

 Dakitari mkuu wa Kitengo cha Macho  Dk. Slim amesema wamefanya matibabu hayo kwa lengo la kuwapunguzia mzingo mkubwa wa gharama kubwa za matibabu ya macho.

P 1Wazazi wa Watoto wenye Miguu Rungu (Clubfoot) Wametakiwa kuwafikisha Watoto wenye matatizo hayo Hospitali kwa ajili ya matibabu ili kuwaepusha na ulemavu wa kudumu.

Hayo ameyasema Mtabibu wa Miguu Rungu ambae pia ni Mtaalamu wa Viungo Bandia ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja Dr. Adil Mussa Haroun amesema kuna baadhi wa wazazi huwafungia ndani watoto wenye matatizo ya miguu rungu na kutowapeleka Hospitali na kudhani kuwa ni ulemavu jambo ambalo sio la kweli kwani tatizo la miguu rungu hutibika na kuondoka kabisa.

 Pia amesema kwa asilimia kubwa tayari watu washaanza kuwa na uwelewa kwani jitihada zao za kutoa mafunzo katika maeneo mbali mbali ya mjini na vijijini kuhusiana na kuwepo kwa Watoto wenye miguu rungu(Club foot) watu hupata muamko na kuwapeleka Watoto wao Hospitali ya Mnazi mmoja kwaajilio ya matibabu.

Hata hivyo amewatoa hofu wazazi kua matibabu yote pamoja na vifaa vya kuwa weka sawa Watoto vinapatikana hospitalini hapo bila ya gharama yoyote .

Kila ifikapo 3 June ya kila mwaka huwadhimisha siku ya miguu rungu(Club foot) duniani lengo ni kutoa elimu na huduma nzuri katika jamiii, ambapo kwa mwaka huu imekuja na kauli mbiu inayosema ‘‘Miguu Rungu si ulemavu kwa hakika inatibika’’.

174101275 123140543195067 5914027656563111390 n

Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja watakiwa kubadilika na kufanya Kazi kwa bidii ili kuimarisha huduma kwa wanao wahudumia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dr.Msafiri L. Marijani wakati akifungua Mafunzo ya Wafanyakazi yanayotolewa na Kitengo cha huduma kwa Mteja yaliyofanyika katika Ukumbi wa Bohari ya madawa ya Hospital hiyo.

Dr Marijani amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uwezo wa utendaji kazi kwa Wafanyakazi hivyo wanatakiwa kuyatumia Mafunzo hayo kwa kutoa mabadiliko chanya ambayo yataimarisha Huduma na kupunguza baadhi ya changamoto zinazojitokeza mara kwa mara kati ya Watoaji Huduma na wanaoihitaji huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambae ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja na Msemaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Hassan Makame Mcha amesema kuwa amewapa Mafunzo hayo Wafanyakazi ili kuimarisha Mawasiliano mazuri na Wanajamii pale wanapohitaji Huduma.

Kwa upande wa Washiriki wa Mfunzo hayo wamesema wameyapokea Mafunzo hayo na kuahidi kubadilika na kuleta Maendeleo ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Mafunzo hayo yametolewa na Kitengo cha Huduma kwa Mteja yalioyowashirikisha Viongozi wakiwemo Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wauguzi wa hospitali ya mnazi.

174264081 123140556528399 6672711888850088868 n

Dr. Msafiri L. Marijani akisisitiza umuhim wa kuyafahamu mafunzo hayo na kuyafanyiakazi kwa wafanyakazi wa Hospitali  kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma mzuri wagojwa wanaofika Hospitali.

Jumuiya ya Watu wenye Uwalbino Zanzibar (JWUZ) wameshauriwa kuzijali sana Afya zao na kuzitunza vyema Ngozi zao hususani katika kipindi cha Jua kali ili kujiepusha na Maradhi ya Ngozi na Magonjwa mengine.

Hayo ameyasema Daktari Bingwa wa maradhi ya ngozi Dr Hafidh S. Hassan  katika Clinic ya maradhi ya Ngozi Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati akitoa huduma kwa wagonjwa wa matatizo ya ngozi wakiwemo Albino.

Aidha Dr. Hafidh amegawa baadhi ya Vifaaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili ya kujikinga na mwanga mkali wa Jua ikiwemo miwani,kofia  pamoja na lotion ambavyo ni muhim kwao kwani Jua huathiri Ngozi zao na Macho.

Nao Viongozi wa Jumuiya hiyo wamewaomba washiriki wenzao kujitokeza kwa wingi katika Clilic yao kwani wanapata kujifunza mambo mengi yanayohusiana na matatizo ya ngozi hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

 Dr.Hafidhi

Daktari Bingwa wa Maradhi ya Ngozi Dr Hafidh S. Hassan, akitoa maelekezo namna ya kujikinga juu ya maradhi ya Ngozi.

alibino1

Baadhi ya watu waliofika katika Clinic ya Ngozi hospitali ya Mnazi Mmoja  wakitoa shukurani za dhati kwa Uongozi wa Hospitali na Madakitari kwa huduma wanazozipata wanapofika clinic.

Ufunguzi wa Majengo Mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto Katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dk Shein.
02 Aug 2020

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Muwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania, Bi Theresia Mcha,alipowasili katika viwanja majengo hayo kwa ajili ya uzinduzi wake. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Ki+kuu cha Haukeland Norway Bwa. Eivind Hansen. wakikata utepe kuashiria kulizindua jengo la Wodi ya Watoto katika eneo la hospitali ya Mnazi Mmoja litakalotoa huduma kwa Watoto na Wazazi katika hospitali hiyo Zanzibar.

Jengo Jipya la Wodi ya Watoto katika hospitali ya Mnazi Mmoja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimsikiliza Muunguzi wa Wodi ya Wazazi akitoa maelezo ya moja ya mashine za kisasa katika jengo hilo zitakazotumika kutowa huduma kwa Wamama Wajawazito katika Wodi hiyo.

Partners

Social media

f  I

Mnazi Mmoja Hospital map Location

Contact us

Mnazi Mmoja Hospital

Stone Town-Vuga Street

P.O.BOX 672

Tel: +255773833768 / +255627600600

Fax: +255 24 2231613

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Web: www.mmh.go.tz